Kwa mujibu wa mwandishi wa Shirika la Habari la Hawza, Ayatullah Sayyid Muhammad Saidi, katika hotuba za Swala ya Ijumaa ya tarehe 14 Shahrivar 1404 katika Musalla ya Quds Qom Iran, alizungumzia nafasi ya mshikamano katika kushindwa kwa mikakati ya maadui, akasema: “Katika mabadiliko ya Asia Magharibi, chumba cha kufikiria cha utawala wa Kizayuni kimekuwa kikiendeleza mkakati mpya; badala ya uvamizi wa moja kwa moja na ukaliaji wa ardhi, kimejikita katika kuleta mitafaruku ndani ya nchi.”
Akaendelea kueleza kuwa: “Mfumo huu wa mashambulizi ni mchanganyiko wa operesheni za kijasusi, vita vya kisaikolojia na mashambulizi ya kijeshi ya kiwango kidogo, ambavyo kwa lengo la kudhoofisha nguzo za uthabiti wa kisiasa na kijamii huendeshwa, kwa fadhila ya Mwenyezi Mungu, njama hii ya adui licha ya ustadi wake, haikufanikiwa, bali imeimarisha mshikamano wa kitaifa na upinzani.”
Imamu wa Ijumaa wa Qom aliongeza kuwa: “Aina hii ya mashambulizi ambayo katika miaka ya karibuni yamejaribiwa Iran, Yemen na Lebanon, badala ya kuzikalia ardhi kifizikia, yamekuwa chanzo cha mshikamano wa wananchi na umoja wao zaidi.”
Akifafanua zaidi, alisema kuwa; Tel Aviv imekuwa ikitumia mbinu zinazojulikana kama “vita mchanganyiko” au “usumbufu wa upole,” zikijumuisha propaganda za kisaikolojia ili kuleta mpasuko wa kijamii pamoja na mashinikizo ya kijeshi, lakini matokeo yake yalikuwa kinyume na matarajio yao.
Ayatullah Saidi alisisitiza kuwa: “Kosa kubwa zaidi la wapanga njama hizi ni kupuuza nafasi kuu ya wananchi katika hesabu za kisiasa na kijamii, walidhani kwa mashambulizi machache na vita vya kisaikolojia wangeweza kuzidisha ufa baina ya serikali na taifa, lakini matokeo yamekuwa tofauti, shinikizo hizi za nje zimekuwa sababu ya kuimarika kwa mshikamano wa kitaifa nchini Iran, Lebanon na Yemen.”
Khatibu wa Ijumaa alisema: “Nchini Iran, kuta imara za mshikamano wa kitaifa na uhusiano wa dhati kati ya wananchi na taasisi za kiserikali zimezima mashambulizi haya ya upole, na kuimarisha roho ya mapambano dhidi ya vitisho vya kigeni.”
Umuhimu wa kuimarisha umoja zaidi ya zamani
Ayatullah Saidi aliongeza kuwa: “Kwa ajili ya kukabiliana na mashambulizi yajayo, kuimarisha mshikamano wa kitaifa ni wajibu mkubwa, mazoezi ya kijamii yenye mhimili wa mshikamo kati ya serikali na wananchi yanaweza kuwa kama ngao ya kisaikolojia Katika uwanja huu mpya, mshikamano wa kitaifa unafanya kazi kama uwanja wa mabomu, kwamba kila hatua ya adui inalipuliwa na mapambano ya wananchi.”
Aidha, kwa mnasaba wa kuzaliwa kwa Mtume (s.a.w.w) na Imam Sadiq (a.s) na wiki ya Umoja, alisema: “Waislamu wa Kisunni wanaona tarehe 12 Rabiul Awwal kuwa siku ya kuzaliwa kwa Mtume (s.a.w.w), na Mashia tarehe 17. Jamhuri ya Kiislamu imeuita muda huu kuwa ‘Wiki ya Umoja’, katika wiki hii, matarajio ya Mtume na Imam Sadiq kutoka kwa Umma wa Kiislamu hukumbushwa.”
Akirejelea Qur’ani, alisema: “Menyezi Mungu anasema katika Suratul Ahzab: ‘Na tumekufanya wewe (ewe Mtume) mwito wa kumwendea Allah kwa idhini yake, na taa ing’arayo kwa ajili ya kuwaongoza watu.’ Pia katika Suratul Anfal: ‘Enyi mlioamini! Itikieni wito wa Mwenyezi Mungu na Mtume wake anapokuiteni kwa mambo yatakayowapa uhai wa kweli.’”
Ayatullah Saidi alibainisha kuwa Mtume (s.a.w.w) kwa ajili ya kuieneza dini ya Kiislamu alichukua hatua tatu:
1. Kuimarisha umoja wa makabila ya Kiislamu.
2. Kuweka undugu baina ya Waumini, kwa mujibu wa Qur’ani (Hujurat:10).
3. Kuanzisha mfumo wa kijamii na sehemu za ibada na mkusanyiko wa Waislamu.
Mwisho, alisema: “Wajibu wetu katika zama za ghaiba ya Imam Mahdi (af) ni kuyakubali matarajio ya Uislamu chini ya kivuli cha mshikamano na utiifu kwa kiongozi wa kidini na Kiongozi Mkuu wa Mapinduzi ya Kiislamu, kwa njia hiyo njama za ubeberu wa kimataifa, hususan Marekani katili na Wazayuni wauaji wa watoto, zitashindwa na kushushwa hadi kwenye udhalili.”
Kwa nini wanafiki walichukizwa na kushuka aya?
Katika khutba ya kwanza, Ayatullah Saidi alizungumza juu ya taqwa na kujisafisha nafsi, akitaja aya ya Qur’ani (Najm:32): “Msijisifie nafsi zenu; Yeye (Allah) ndiye anayejua zaidi nani ni mchamungu.”
Alisema: “Mtu akijitahidi kweli kujisafisha nafsi, akitembea katika njia ya nafsi yake kwa mwanga wa akili na Sheria, atakuta maovu mengi kiasi kwamba hatopata muda wa kuangalia makosa ya wengine, Imam Ali (a.s) amesema: ‘Bora ya watu ni yule ambaye makosa yake mwenyewe yanamshughulisha kiasi cha kutompa nafasi ya kuchunguza makosa ya watu wengine.’”
Kisha akagusia aya ya Qur’ani (Tawbah:127) inayohusu wanafiki walipokuwa wakikerwa na kushuka kwa aya mpya, na mara kwa mara waliondoka kwa siri wakati Qur’ani inasomwa, akasema: “Wanafiki walificha usaliti wao dhidi ya Mtume, walihofia kufedheheshwa mbele ya watu lakini hawakuwa na woga wa kufedheheshwa mbele ya Mungu, hii ndiyo alama ya unafiki na kutokuwa na imani ya kweli.”
Mwisho aliongeza: “Mikakati ya wanafiki haikomi. Kwa njia ya dhihaka kwa aya za Mwenyezi Mungu, wanapunguza hadhi ya Qur’ani, kumkosea heshima Mtume (s.a.w.w), kudharau kikao cha kushuka kwa aya, na kuwaudhi Waislamu.”
Maoni yako